Simba abeba ubingwa, Stand United, African Lyon zashushwa

Pazia la Ligi Kuu ya kandanda Tanzania bara imefikia tamati Jumanne kwa michezo 10 kuchezwa katika viwanja tofauti tofauti, michezo iliyokuwa inatazamwa zaidi ni ile yenye kuamua nani kushuka daraja na nani kucheza mchezo wa mtoano.
Amani Sports News tunakuletea timu hizo.
Kwa upande wa bingwa wa ligi Kuu tayari klabu ya Simba imeshafanikiwa kulibakiza taji hilo mitaa ya Msimbazi kwa kufikisha alama 93 ambazo zisingefikiwa na timu yoyote.
Changamoto kubwa ilikuwa timu yenye kuamua kushuka daraja kwa kuungana na African Lyon mwenye pointi 23.
Katika michezo iliyopigwa leo klabu ya Stand United kutoka Shinyanga yenye pointi 44 zimeshuka daraja moja kwa moja na kuungana na Lyon ya Zamunda.
Kagera Sugar ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 44 ikiwa na tofauti ya mabao ya kufungwa ambapo Stand United wamefungwa jumla ya mabao 50 na Kagera Sugar imefungwa jumla ya mabao 43.
Mwadui FC imemaliza ikiwa nafasi ya 17 hivyo nayo itacheza mchezo wa mtoano(Playoff) kama Kagera Sugar.
Matokeo ya leo kiujumla ni haya hapa:-
Matokeo kwa ujumla.
FT: Coastal Union 0-0 Singida United.
FT: Mbeya City 0-0 Biashara United.
FT: Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC.
FT: Ruvu Shooting 1-0 Alliance FC (Fully Zullu Maganga 25’ p) .
FT: JKT Tanzania 2-0 Stand United (Samweli Kamuntu 51’, Najimu Maguli 73’).
FT: Ndanda SC 1-3 Mwadui FC (Kigi Makasi : Ottu Joseph 39’, 41’, Salim Aiyee 61’) .
FT: Yanga SC 0-2 Azam FC (Daniel Amoah 45’+2, Mudathir Yahya 50’).
FT: Mbao FC 1-1 Kagera Sugar (Hebert Lukindo 60’ : Ally Ramadhan 20’).
FT: Tanzania Prisons 3-1 Lipuli FC (Benjamini Asukile 29’, Adam Adam 48’, 85’ : Seif Rashid 46’).
FT: African Lyon 0-2 KMC FC (Cliff Buyoya 21’, 17’)

Author: Bruce Amani