Simba Day yatajwa kuja kipekee

Kaimu msemaji wa Simba SC, Ezekiel Kimwaga leo Septemba 3, 2021 amesema kuwa kuelekea katika kilele cha Simba Day inayotarajiwa kufanyika Septemba 19 wanakuja na kauli mbiu itakayotumika pamoja na viingilio.

Kamwaga akiongea na Wanahabari katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam amesema kilele cha Simba Day kitakuwa cha kipekee.

Kimwaga, ametangaza bei za viingilio kwenye Simba Day itakayofanyika mwezi huu Septemba 19, katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

Kwa upande wa Platinum Tsh. 200,000, VIP Tsh 30,000, VIP B&C Tsh 20,000 na mzunguko ni Tsh 5,000.

“Slogan ya Simba Day 2021 ni One Team, One Dream tukimaliza na Asubuhi Tu, Twendeni Wenye Nchi.

“Maandalizi yapo vizuri na kwa sasa niwaombe mashabiki nguvu na macho yote tuelekeze kwenye tamasha letu ambalo litakuwa ni nzuri na lenye upekee,”

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares