Simba haikamatiki, yaichapa Namungo FC 3-2

Simba imeibuka kidedea dhidi ya Namungo FC kwa goli 3-2 katika mchezo wa TPL uliopigwa dimba la Taifa leo Jumatano.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba walikuwa ya kwanza kuandikisha goli la kuongoza kupitia kwa Francis Kahata kunako dakika ya 21 ya mchezo akimalizia pasi ya Shomari Kapombe mlinzi wa kulia wa Simba, strika wa Namungo Bigirimana Blaise anasawazisha goli hilo kabla ya Dilunga kufunga tena goli ya 2 kwa Simba na mpaka timu zinaingia kwenye mapumziko Simba 2-1 Namungo.

Kipindi cha pili Namungo walipata bao la pili kupitia kwa Lusajo ambaye aliachia shuti kali akiwa nje ya 18 alichoambulia Kakolanya ilikuwa kuokota mpira nyavuni.

Dakika ya 88, Kagere alimaliza shughuli uwanjani wa Taifa kwa kufunga bao la ushindi ambalo limewapa Simba pointi tatu jumla.

Sasa Wekundu wa Msimbazi Simba inafikisha jumla ya alama 44 ikiwa nafasi ya kwanza na imefunga jumla ya mabao 38.

KWINGINEKO

Polisi Tanzania imetoka kifua mbele kwa kuichapa Tanzania Prisons goli 1-0 ukiwa ni mwendelezo wa TPL.

Author: Bruce Amani