Simba kibaruani Afrika Kusini mbele ya Kaizer Chiefs Ligi ya Mabingwa

298

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara VPL klabu ya Simba Leo Jumamosi Mei 15 saa moja usiku itashuka dimbani kumenyana vikali dhidi ya wenyeji wao Kaizer Chiefs katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali mkondo wa kwanza.

Simba inayonolewa na kocha Didier Gomes Da Rosa ina kibarua kizito kutokana na uzoefu wa mpinzani wake Chiefs ambaye hayuko kwenye kipindi kizuri kiubora uwanjani lakini ina historia kubwa ya soka la Afrika pamoja na Uwekezaji mkubwa.
Akizungumzia mchezo huo, kocha Didier Gomes amesema anafahamu utakuwa mchezo mgumu lakini wako tayari kupambana kuangalia kama watapata matokeo chanya.
Licha ya maneno ya kocha bado kuna hati hati ya kuwakosa baadhi ya nyota wake Ally Salim kipa namba tatu, Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael bado hawajawa fiti asilimia 100 kwa ajili ya mchezo wa leo.
John Bocco ambaye ni nahodha wa Simba imeelezwa kuwa ana asilimia 50 kuanza ama kutokuanza kwa kuwa bado hajawa fiti.
Miraj Athuman na Said Ndemla hawa wameachwa Bongo kutokana na sababu mbalimbali huku Perfect Chikwende yeye hajasajiliwa kwa mashindano ya kimataifa yupo kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara.

Author: Asifiwe Mbembela