Simba, KMC uwanjani Leo kusaka pointi tatu VPL

432
Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara inaingia mzunguko wa pili leo Ijumaa ambapo kutakuwa na michezo miwili, dimba la Uhuru Dsm Simba itacheza na Mtibwa Sugar wakati ambao KMC itakuwa ugenini dhidi ya Coastal Union.
Simba Sc inaweza kuingia kwenye mchezo huo na uhakika wa ushindi kutokana na historia nzuri iliyonayo kwa Wavuna miwa wa Mtibwa Sugar kutoka Morogoro.
Katika michezo 10 ya mwisho kati ya timu hizi, Simba imeshinda mara 6 na kufunga goli 11 wakati ambapo michezo minne imeenda kuwa sare au suluhu, Mtibwa haijaambulia kitu.
Simba itamkosa Nahodha John Bocco (majeruhi), huku Deo Kanda kukiwa na asilimia fulani za kuukosa mtanange huo.
Mtibwa itakuwa chini ya kocha msaidizi kutokana na kocha mkuu Zubery Katwila kuwa katika majukumu ya taifa, yupo na kikosi cha timu ya taifa chini ya miaka 20.
Kwingineko.
Kocha Juma Mgunda atajiuliza alikosea wapi  pale timu yake ya Coastal Union ilipokubali kipigo cha goli 5-1 dhidi ya Kino Boys mchezo wa msimu uliopita, pale ambapo watakuwa wenyeji wa KMC leo Ijumaa katika dimba la Mkwakwani Tanga.
KMC ilifungwa mchezo wa kwanza wa Ligi dhidi ya Azam, hali kadhalika kwa Coastal Union ilipoteza kwa Polisi Tanzania.

Author: Bruce Amani