Simba kucheza Kigoma mechi za kirafiki

Simba Sports Club itacheza mechi mbili za kirafiki katika kujiweka sawa kiushindani hasa kipindi hiki ambapo kuna kalenda ya FIFA ya michuano ya kimataifa.
Simba ambayo ni mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara itazicheza mechi hizo mkoani Kigoma, dhidi ya dhidi ya Mashujaa Fc mtanange utakaopigwa Oktoba 09 siku ya Jumatano.
Baada ya mchezo huo Simba itaendelea kusalia mkoani Kigoma ambapo Oktoba 11 Ijumaa itacheza na Aigle Fc, mabingwa wa Burundi
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema michezo hiyo itawasaidia kuiweka timu katika hali ya ushindani wakati huu ambao ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA
Wachezaji ambao hawakuitwa timu za Taifa watahusika kwenye michezo hiyo ambapo licha ya kuendeleza ushindani pia hutoa nafasi kwa kocha kutathimini ubora wa wachezaji wanaokosa namba kwenye kikosi cha kwanza
Michezo ya Ligi Kuu itaendelea Oktoba 23 kwa Simba kuikabili Azam Fc.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends