Simba kuchuana vikali na Kaizer Chiefs robo fainali Ligi ya Mabingwa

Shirikisho la Kandanda barani Afrika – CAF limekamilisha upangaji wa ratiba ya michezo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ya hatua ya robo fainali ambapo wawakilishi wa Tanzania Simba wamepangwa dhidi ya Kaizer Chiefs.

Kwenye Droo hiyo iliyofanyika Leo Ijumaa Aprili 30, Cairo, Misri, CAF imetumia utaratibu ule ule wa kawaida wa timu zilizotoka kundi moja haziwezi kukutana, na timu nchi moja kuna uwezekano wa kukutana.
Simba wataanzia ugenini nchini Afrika Kusini katikati ya tarehe 14 na 15 ya mwezi wa tano kabla ya kurejea tena wiki moja baadaye ya Mei 21au 22 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwenye michuano hiyo msimu huu, Simba haijapoteza mchezo wowote kwenye uwanja wa Mkapa jambo ambalo limepekekea baadhi ya wananchi wa Afrika Kusini kupata hofu na Simba hasa ugenini (kwa Mkapa).
Mbali na Simba, droo nzima iko hivi:-
Al Ahly Vs Mamelodi Sundowns
CR Belouizad Vs Esperance des Tunis
MC Alger Vs Wydad Casablanca na Simba Vs Kaizer Chiefs. 

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares