Simba kuelekea Afrika Kusini kwa maandalizi ya msimu

Simba inategemea kuondoka nchini siku ya Jumatatu Julai 15 kuelekea Afrika Kusini ambako inaenda kuweka kambi ya takribani wiki tatu kujiandaa na msimu mpya wa 2019/20.  Kuekea msimu huo mpya Wekundu wa Msimbazi Simba wametoa mpangilio wa namba za jezi kwa wachezaji wake.

Nahodha wa Yanga msimu uliopita Ibrahim Ajib Migomba amepewa jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na Adam Salamba. Ikikumbukwe pia Ajib alikuwa anatumia namba 10 akiwa na Yanga.

Ukiachana na wachezaji wapya, kuna baadhi ya wachezaji wa zamani ambao wamebadilishiwa namba, kama chipukizi Rashid Juma amepewa namba 16 iliyokuwa ikitumiwa na Shiza Kichuya. Msimu wa 2018/2019 Rashid Juma alikuwa akitumia namba 35.

Orodha kamili hii hapa:-

Ibrahim Ajib – 10
Kennedy Juma – 26
Walker Henrique Da Silva 11
Tairone Santos da Silva – 3
Gadiel Michael – 2
Deo Kanda – 7
Sharaf shiboub – 8
Gerson Fraga Viera – 4
Fransis Kahata – 25
Miraj athuman – 21
Beno Kakolanya – 30

Katika msimu wa 2019/20 Simba itashiriki mashindano mbalimbali kama Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu Tanzania bara, FA, Kombe la Mapinduzi na Sportpesa Supercup.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends