Simba kujaribu mastaa wake kwa African Sports

Kikosi cha Simba kitamenyana na African Sports kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa katika dimba la Azam Complex jijini Dar es Salaam leo Novemba 16. Wekundu wa Msimbazi Simba inayonolewa na Kocha mkuu Sven Vandenbroeck inatazamia mchezo huo kuangalia wachezaji wapya ambao hawapati nafasi.

Kwenye mtanange wa leo viingilio ni 3,000 kwa mzunguko na elfu tano kwa VIP, ambapo mtanange huo utaanza kuchezwa kuanzia majira ya saa 1 usiku.

Author: Asifiwe Mbembela