Mbabane Swallows kutua Dar kupambana na Simba

Mabingwa wa soka nchini Swaziland Mbabane Swallows wanataraji kutua leo jijini Dar-es-Salaam tayari kwa mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya wenyeji wao ambao pia ni mabingwa wa soka Tanzania Wekundu wa Msimbazi Simba Jumatano hii ya Novemba 29 katika dimba la Taifa jijini Dar -es – Salaam

Simba ambayo kwa miaka kadhaa imekosekana katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika inaonekana ina kiu kubwa ya kufanya vyema msimu huu katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu

Mbabane wanakumbukwa na mashabiki wa soka hasa wale wa Azam baada ya timu hiyo kuibana Azam katika uwanja wa Chamazi na kulazimisha sare kabla ya timu hiyo kuifunga Azam kwa magoli 3 – 0 na kuitoa katika michuano ya kombe la Shirikisho misimu mitatu iliyopita

Simba ambayo bado inaonekana kusuasua katika michezo ya ligi kuu kwa kukamata nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na Azam imeripotiwa kusahau kuhusu ligi kuu na sasa wameelekeza nguvu zao zote katika michuano ya kimataifa ili msimu huu wafanye vyema kama ilivyo ada kwa upende wao hasa katika michunao ya kimataifa

Akikaririwa Jijini Dar-es-Salaam kiungo fundi wa Wekundu hao wa Msimbazi Simba Jonas Gerard Mkude amesema wapo kamili kuwavaa wa Swaz hao siku ya juma tano hivyo kuwataka mashabiki kujitokeza kuwaunga mkono mabingwa hao wa soka Tanzania

“Tupo vizuri wachezaji wote na tunatambua kuwa kazi iliyo mbele yetu ni kubwa, tunaomba Mungu tuweze kupata matokeo kwa kuwa hayo ndio malengo yetu kuweza kushinda mchezo wetu wa kimataifa.

“Jumatano tutakuwa uwanjani, mashabiki wajitokeze kwa wingi maana wana umuhimu sana katika kufanikisha ushindi, watanzania kwa pamoja watupe sapoti katika mashindano haya ya kimataifa hatutawaagusha,” alisema Mkude.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends