Simba kuvaana na Coastal Union

Mabingwa watetezi wa VPL Simba watakuwa katika Uwanja wa Uhuru kuwakaribisha vijana wa Juma Mgunda Coastal Union katika mtanange unaotarajiwa kuwa ni wa kukata na shoka kwa timu zote mbili kutokana na vita ya kuwania ubingwa inayoendelea hivi sasa.

Simba ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 44 baada ya kucheza mechi 17 itakutana na Coastal Union iliyo nafasi ya tatu na pointi zake 30 baada ya kucheza mechi 17 pia.

Rekodi zinaonyesha kuwa kwa msimu uliopita wa 2018/19 ambao Coastal Union ilipanda daraja iliambulia kichapo mechi zake zote mbili mbele ya Simba jambo litakaloongeza ugumu kwa timu zote.

Mchezo uliochezwa Dar, Uwanja wa Uhuru, Simba ilishinda mabao 8-1 na ule uliochezwa Tanga, Mkwakwani Simba ilishinda mabao 2-1.

Jumla Coastal Union ilifungwa mabao 10-2 na kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, wachezaji wawili walifunga hat trick kutoka Simba ambao ni Emanuel Okwi na Meddie Kagere.

Sven alisema kuwa anahitaji kuona wachezaji wakipambana kupata pointi tatu, huku Juma Mgunda wa Coastal Union akisema kuwa hana mashaka na uwezo wa wachezaji dakika tisini zitaongea.

KWINGINEKO VPL LEO JUMAMOSI

Namungo v Mbao, Majaliwa.

Ndanda v Alliance, Nangwanda.

Kagera Sugar v Singida United, Kaitaba.

Biashara V Mwadui, Karume.

Ruvu v Lipuli, Isamuhyo.

Prisons v KMC, Jamhuri.

Simba v Coastal Union, Uhuru.

Mbeya City v Azam, Samora

Mechi zote zitaanza saa 10 jioni

Author: Bruce Amani