Simba kuvaana na JKT uwanja wa Taifa

Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba, kesho Jumatano atashuka Uwanja wa Taifa kumenyana na Polisi Tanzania mchezo wa Ligi Kuu utaopigwa dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo utakuwa wa 19 kwa Simba kukamilisha mzunguko wa kwanza sawa na Polisi Tanzania ambao wote wanamaliza mzunguko wa kwanza tangu ligi hiyo kuanza mwezi wa nane.

Mechi zao zote mbili za mwisho wameshinda ambapo Simba ilishinda mabao 2-0 mbele ya Coastal Union na Polisi Tanzania ilishinda bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania.

Sven Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hesabu kubwa ni kupata ushindi utakaowafanya wazidi kuongeza nguvu ya kutafuta ubingwa na Malale Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa watapambana kupata ushindi

Simba wataingia kwenye mchezo huo kukamilisha ratiba ya mazunguko wa kwanza ambapo ikishinda itakuwa na alama 50 katika nafasi ya kwanza wakati JKT itakuwa na alama 29 nafasi ya

Author: Bruce Amani

Facebook Comments