Simba kuwakaribisha wakata miwa wa Moro

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Simba sc inaingia uwanjani kucheza dhidi wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara mchezo utakaofanyika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam, majira ya 10 jioni.

Simba imeshindwa kupata alama tatu kwenye michezo miwili iliyopita, imepoteza mmoja(Kagera) na imetoa sare na (Azam) hivyo watakuwa wanahitaji ushindi kurudisha matumaini ya ubingwa na furaha ya mashabiki.

Simba wanaingia kwenye mchezo huo ikiendelea kuwakosa wachezaji wao muhimu kutokana na majeruhi yanayoikabili timu hiyo.

Pascal Wawa, Shomary Kapombe, na Asante Kwasi wataukosa mtanange wa leo, licha ya kuanza mazoezi binafsi.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema wao kama Mtibwa hawapo tayari kuwa daraja la Simba kutwaa Ubingwa hivyo Simba isitegemee mteremko kwenye mtanange huo, ambao ni mchezo wa mkondo wa kwanza.

“Sisi sio daraja, tumeshindwa kufanya vizuri katika mechi za karibuni tunahitaji kushinda na kupata alama tatu leo ili kuendelea kujiweka sehemu nzuri, hatutakubali kupoteza kiurahisi, alisema Tobias Kifaru.

Simba wamebakiza mechi tano kumalizika kwa msimu wa 2018/2019 katika michezo hiyo inahitaji alama nane, endapo watapata kwenye mchezo wa leo pointi tatu basi watajitengenezea mazingira ya ubingwa

Mechi zilizobaki za Simba ni pamoja na Mtibwa Sugar (leo), Biashara United, Singida United, Mtibwa Sugar, na Ndanda Fc.

Matokeo ya TPL Mei 15

* Biashara 1-2 Alliance Fc.

Author: Bruce Amani