Simba mwendo mdundo, KMC yachechemea

272

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa dimba la Uhuru jijini Dsm.

Ushindi huo umepatika kupitia mabao ya Meddie Kagere dakika ya 17 kipindi cha kwanza na Miraji Athumani akifunga dakika ya 68 kipindi cha pili, magoli yakionekana pande zote zilikosa umakini katika safu ya ulinzi.

Kabla ya Miraji kuongeza bao la pili, kipindi cha kwanza Riffat Khamis aliisawazishia Mtibwa dakika ya 20 ikiwa ni dakika tatu pekee Kagere acheke na nyavu na matokeo kuwa 1-1.

Ushindi huo umewafanya Simba kufikisha jumla ya alama sita wakiwa kileleni mwa ligi.

MATOKEO MENGINE

Wakati huo, KMC nao waliokuwa ugenini dimba la Mkwakwani Tanga kucheza dhidi ya Coastal union wamelala kwa mabao 2-0 kutoka kwa Wagosi hao wa Kaya, unakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa KMC kupoteza, wakati Coastal Union ikiwa imeinuka baada ya kupoteza mechi ya awali.

Author: Bruce Amani