Simba na Clatous Chama kamili gado kuwavaa Al Ahly CAFCL

Klabu ya Simba imesema nyota wake Clatous Chota Chama ambaye ni kiungo mshambuliaji yuko fiti asilimia 100 hii ni kuelekea mtanange wa kesho Jumanne katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Taarifa ya kuwa salama kwa kiungo mshambuliaji Chama zinakuja baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa nyota huyo anasumbuliwa na majeruhi ambayo awali ilikuwa inaelezwa kuwa huenda yangemfanya kuukosa mchezo wa kesho wa CAFCL.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa kwenye kila nchi kuna mtawala na mfalme wake hivyo kwa upande wa Simba mfalme ni Chama.

“Chama akiwa bora ndani ya uwanja anaifanya timu iwe na kasi katika kusaka matokeo ambayo timu inahitaji.

“Kila timu ina mwenyewe, ushindi wa Simba Chama akiwa kwenye ubora wake basi ujue hatufungwi kwa namna yoyote na timu yoyote,”

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares