Simba na Yanga zaanza msimu kwa ushindi

72

Ligi kuu ya Tanzania bara, ilianza wiki hii kwa mechi kadhaa kuchezwa nchini humo. Ligi ya msimu huu, inashirikisha timu 20, na imeanza bila ya kuwepo kwa mdhamini Mkuu. Mabingwa watetezi Simba FC walianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons. Matokeo mengine yaliyoshuhudiwa siku ya kwanza, Kagera Sugar 2-1 Mwadui, Biashara United 1-0 Singida United, Mbao 1-0 Alliance, Yanga 2-1 Mtibwa Sugar, Azam 2-0 Mbeya.

Author: Bruce Amani