Simba Queens yaanza vyema Ligi ya Mabingwa Afrika Mashariki

Kikosi cha Simba Queens kimepata ushindi mnene wa goli 4-1 dhidi ya PVP FC katika mchezo wa kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake ukanda wa Afrika Mashariki, mtanange uliopigwa dimba la Nyayo Jijini Nairobi Kenya mchezo wa Kundi A.

Mabao ya Simba Queens yamefungwa na beki Mzimbabwe, Danai Bhobho dakika ya 10, winga Mkongo Flavine Mawete Musolo dakika ya 32 na 81 na mshambuliaji mzawa, Aisha Juma Mnunka dakika ya 84.

Simba Queens itashuka dimbani kwa mara nyingine Jumanne kumenyana na Lady Doves WFC ya Uganda, kabla ya kukamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na FAD FC ya Djibouti Ijumaa Septemba 3.

Bingwa atashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwaka huu nchini Misri, ambayo itahusisha timu nane, nyingine kutoka kanda nyingine barani zitakazogawanywa katika makundi mawili.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares