Simba SC yaanza ilipoishia, yailaza Ihefu 2 – 1

39
Klabu ya Simba imeanza pale ilipoishia kufuatia kujipatia ushindi wa bao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini VPL katika mtanange uliopigwa dimba la Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya ikiwa ni mechi za mwanzo kabisa ya kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu.
Simba ambao wanaingia kwenye msimu huu 2020/21 wakiwa mabingwa watetezi kufuatia kutwaa taji hilo mara tatu walitangulia kujipatia bao la kuongoza kupitia kwa nahodha wa kikosi hicho John Raphael Bocco akimalizia pasi ya Mzamiru Yasni katika ungwe ya kwanza ya mchezo.
Ihefu walirudi dakika chache ungwe ya kwanza na kusawazisha goli hilo wakitumia makosa vema ya walinzi wa Simba waliongozwa na Joash Onyango na Kennedy Juma goli lililofungwa na Omary Mponda kwenye dakika ya 15 dakika tano pekee baada ya goli la Simba.
Ungwe hiyo hiyo ya kwanza klabu ya Simba ilikuwa ilijipatia bao la pili kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na mchezaji bora wa msimu raia wa Zambia Clatous Chota Chama na kumaliziwa na Mzamiru Yasni kunako dakika ya 42 kipindi cha pili.
Ihefu ambayo imepanda daraja msimu huu imefanikiwa kuonyesha uwezo mzuri licha ya kutofanikiwa kuondoka na alama tatu ambazo zimeenda kwa Wekundu wa Msimbazi lakini wameonekana wakiendelea hivyo wanaweza kuwa washindani haswa wa VPL.
Matokeo mengine;
Namungo FC 1-0 Coastal Union
Dodoma Mji 1-0 Mwadui FC
Mtibwa Sugar 0-0 Ruvu Shooting
Biashara 1-0 Gwambina FC

Author: Asifiwe Mbembela