Simba, Vita Club hapatoshi kwa Mkapa, Al Ahly na Merrikh waangushana pia

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Tanzania klabu ya Simba inashuka dimbani leo Jumamosi Machi 3 kumenyana vikali dhidi ya AS Vita Club ya Congo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, mtanange utakaopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.

Simba ambao ni vinara wa Kundi A ambalo lina bingwa mtetezi wa taji la Ligi ya Mabingwa Al Ahly, ina alama 10 ambapo kwenye mechi mbili zilizosalia inahitaji alama moja pekee kufuzu kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa ngazi ya klabu.
Kwa upande wa, Vita Club alama tatu ni muhimu kwani ina alama nne ambazo zitakosa maana endapo watashindwa kuvuna ushindi leo Jumamosi mbele ya Simba ambayo haijapoteza wala kutoa sare katika uwanja wa Mkapa mechi ya makundi.
Hata hivyo, kukosekana kwa nyota kama Shaban Djuma wa AS Vita kunainyong’onyesha klabu hiyo inayonolewa na kocha Ibenge.
Mbali na mchezo wa Simba dhidi ya Vita, mtanange mwingine wa kundi hilo utakuwa kati ya Al Ahly waliosafiri kutoka Misri mpaka Sudan kuchuana na El Merrikh wenye alama moja.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares