Simba Wafanya Mazoezi ya Kwanza Casablanca

83

Kikosi cha Simba baada ya kutua salama Casablanca kimefanya mazoezi ya kwanza kujiwinda na mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Wydad Casablanca mchezo utakaochezwa uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca Ijumaa Aprili 28.

Wekundu wa Msimbazi wako Morocco wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri hasa wakibebwa na bao moja ambalo walilipata wakicheza uwanja wa nyumbani likifungwa na Jean Baleke.

Mchezo huo utachezwa saa nne usiku.

Author: Asifiwe Mbembela