Simba Walalamika Kuhujumiwa, Nani aliyevujisha Jezi?

Kaimu Afisa Habari wa Simba amejiuliza ni nani ambaye amevujisha jezi zao siku moja kabla ya utambulisho wake rasmi.

Kwa madai yake amehusisha na upande wa pili kwa maana ya Watani wa Jadi ingewaa hajawataja wazi, maana anasema “tunaweza kuhama kwenye utani wa jadi kwenda kwenye uhasama, jambo ambalo si nzuri”.

Baada ya jezi kuvuja, Simba imeweka wazi kuwa kwa sasa jezi mpya kwa msimu wa 2021/22 zinapatikana kwenye maduka yote ya Vunja Bei ambao ni wazalishaji wa jezi hizo.

Ezekiel Kwamwaga, Kaimu Ofisa Habari wa Simba amesema kutokana na maombi ya mashabiki wengi wa Simba kuzihitaji jezi hizo wakaona hakuna tatizo wakaamua kuziruhusu zipatikane madukani.

“Awali ilikuwa tumepanga kuzindua rasmi Septemba 4 kutokana na maombi ya mashabiki wengi wa Simba tumeamua kuziruhusu kupatikana katika maduka ya Vunja Bei.

“Ni jezi nzuri na bora na kila shabiki ajivunie na apate jezi yake orijino nina amini kwamba hakuna ambaye ataweza kupenda kuona anavaa kitu feki hilo halipo hivyo kila mmoja ajipatie jezi mpya.

“Kuhusu uzinduzi siku ya Jumamosi bado upo palepale na tutatoa utaratibu namna mambo yatakavyokuwa ni suala la kusubiri na kuona,”

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares