Simba wampata kocha mkuu mpya

101

Baada ya ngoja ngoja ya muda mrefu, hatimaye ni rasmi kwamba Wekundu wa Msimbazi Simba SC wamepata kocha mpya. Mabingwa hao wa Tanzania Bara wamemtangaza Mbelgiji Sven Vanderbroeck mwenye umri wa miaka 40 kuchukua mikoba ya ukufunzi kutoka kwa Mbelgiji mwenzake aliyetimuliwa Patrick Aussems.

Sven aliwahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Cameroon – The Indomitable Lions iliyotwaa Ubingwa waa AFCON 2017 nchini Gabon.

Aidha Mbelgiji huyo amewahi kuwa kocha mkuu wa Chipolochipolo wa Zambia kuanzia 2018 hadi 2019. Simba hawajaweka wazi wameingia mkataba wa muda gani na Sven, ambaye pia aliwahi kucheza soka katika vilabu kadhaa nyumbani Ubelgiji ikiwemo Mechelen.

Author: Bruce Amani