Simba watua salama Dar kujiandaa na Ligi ya VPL baada ya kibarua ya Ligi ya Mabingwa Afrika

294

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Tanzania Wekundu wa Msimbazi Simba wamerejea salama nchini baada ya kulazimisha sare tasa dhidi ya Al-Merrikh ya Khartoum Sudan.

Simba inaongoza kundi A la michuano hiyo na pointi zao saba, huku ushindani ndani ya kundi hilo ukizidi kuwa mkubwa katika kusaka nafasi ya kwenda hatua ya robo fainali.

Al Ahly na AS Vita baada ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 wamefikisha jumla ya pointi nne huku Al Merrikh wao wakiwa wanaburuza mkia na pointi yao moja.

Author: Asifiwe Mbembela