Simba yabanwa nyumbani na TP Mazembe

Simba SC imetoshana nguvu na TP Mazembe ya 0-0 kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika katika mtanange uliochezwa uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Jumamosi hii.

Katika mchezo huo Simba hawana budi kujilaumu wenyewe kwa kukosa umakini katika kumalizia nafasi kadhaa walizozitengeneza, Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi wote walipata nafasi nzuri ya goli ingawa umakini haukuwepo.

Kwa upande wa Mazembe walioonekana kucheza kwa tahadhari ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinaisha walikuwa chini katika umiliki wa mpira kwa asilimia 54 kwa 46 ingawa walikuwa wanaongoza kwa majaribio.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya CAF msimu huu Simba kushindwa kufunga goli hata moja katika uwanja wa taifa/Mkapa tangu hatua ya mtoano, makundi mpaka robo fainali kupigwa mpaka sasa.

Huenda Simba ingeweza kupata alama 3 katika dakika ya 59 baada ya kupata penati iliyopigwa na Nahodha John Bocco kupaa juu ya mtambaa wa panya.

Dakika tisini ziliashiria mpira ni sare (0-0) ambayo ina lazimisha Simba kucheza kwa kufa au kupona kuhakikisha inapata hata alama moja ugenini Lubumbashi licha ya kutokuwa mchezo rahisi.

Ina maana kwamba Simba inahitaji ushindi wowote, au sare ya magoli mengi ili ifuzu ingawa timu kutoka Uarabuni amekufa 8-0.

Aidha, TP Mazembe itarudiana na Simba wiki ijayo kwa ajili ya kukamilisha ratiba ya robo fainali ya mashindano hayo yenye heshina kubwa Afrika kwa ujumla.

Mwekezaji wa timu ya Simba amekaririwa mara kadhaa akisema Simba itafikia kuwa mabingwa siku moja. Mohammed Dewji anajua thamani ya uwekezaji wake pindi Simba ikitwaa taji hilo.

Mchezo mwingine.

Mamelody Sundowns 5 – 1 Al Ahly

 

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends