Simba yaiduwaza Al Ahly kwa Mkapa, yaichapa 1-0 Luis Miquissone atambaa

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Tanzania na washiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika Simba SC wamefanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Leo Jumanne kwa Simba kushinda bao 1-0.

Goli pekee katika mechi hiyo, limefungwa na winga hatari Luis Miquissone kwa shuti kali akimalizia mpira wa kiungo mshambuliaji Clatous Chota Chama kwenye dakika ya 29 ya mchezo.

Simba ambayo iliingia kwenye mechi hiyo na kauli mbiu ya “Total War in Dar. Point Of No Return” inafikisha alama sita katika mechi mbili ambazo wamecheza, walianza kupata ushindi ugenini nchini Congo dhidi ya AS Vita kabla ya ushindi wa leo, mechi zote imeshinda kwa bao moja moja.

Kitakwimu klabu ya Simba katika mechi hiyo waliongoza kila kitu kuanzia umiliki wa mchezo, mashuti ya golini na kona pia.

Simba inakuwa timu ya pili kuifunga klabu ya Al Ahly tangu kocha Pitso Mosimane kocha wa kwanza alikuwa ni Hans Flick akiwa na Bayern Munich ya Ujerumani.

Mbali na matokeo ya uwanja wa Mkapa, AS Vita wakiwa ugenini nchini Sudan wameshinda goli 4-1 dhidi ya El Merreikh na kukamata nafasi ya pili chini yao akiwa Al Ahly wakiwa sawa alama (tatu) wa mwisho akiwa ni El Merreikh akiwa hana pointi sifuri.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares