Simba yaikata Mbao katika dimba la CCM Kirumba

20

Mabingwa watetezi wa TPL Simba SC wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Wabishi Mbao FC ya Mwanza katika mtanange uliopigwa dimba la CMM Kirumba leo Alhamis, Jan 16.

Ikiwa na maumivu ya kupoteza mchezo wa fainali ya Mapinduzi Simba ilianza kuandikisha goli la kwanza kupitia shuti la mguu wa kushoto Hassan Dilunga ‘HD’ kunako dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza akimalizia pasi ya Jonas Gerrard Mkude.

Bao hilo liliwapeleka Simba mapumziko wakiwa mbele huku Mbao FC wakienda kujipanga kupindua meza kibabe kwenye mchezo wa leo ambao ulichezwa kwenye Uwanja wenye maji kutokana na changamoto ya mvua.Kipindi cha pili Mbao iliyo chini ya Hemed Moroco walijipanga upya kabla ya kuanza kuonyesha kasi yao Jonas Mkude aliongeza uzito kwa kufunga bao lake la kwanza msimu huu kwa shuti kali akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu na kuwafanya Simba kuwa mbele kwa mabao 2-0.

Mbao FC hawakuwa wanyoge walirejea mchezoni na dakika ya 52 walifunga bao la kufutia machozi akiwa katikati ya mabeki wa Simba na kuwarejesha kwenye mchezo Mbao.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 38 ikiwa nafasi ya kwanza ndani ya ligi kwa sasa ikiwaacha wapinzani wao Yanga 13 ikiwa imecheza mechi 13 na ina michezo miwili kuwa sawa na Simba kwa sasa ina pointi 25.

Kipi kinafuata?
Simba itaendelea kusalia jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo dhidi ya Alliance tarehe 19 mwezi Januari huku vijana wa Hemmed Morroco Mbao wakisafiri mpaka Lindi kumenyana vikali dhidi ya Namungo

Author: Bruce Amani