Simba yailipa Yanga kwa Peter Banda wa Malawi

821

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Wekundu wa Msimbazi Simba wamempa mkataba wa miaka mitatu winga wa kimataifa wa Malawi, Peter Banda ambaye alikuwa anakipiga kwa mkopo ndani ya Klabu ya Sheriff ya Moldovia.

Winga huyo ambaye amejiunga na Simba Leo Agosti 3, huku ikielezwa kuwa amekuja Simba kwa ajili ya kuziba nafasi ya Luis Miquissone anayetajwa kuwindwa na miamba ya soka la Afrika klabu ya Al Ahly ya Misri.

Simba ambao tangu Jana Jumatatu walikuwa wametoa taarifa kuwa watamtambulisha mchezaji mpya ingawa Leo rasmi mchezaji huyo ametambulisha kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

Awali mchezaji huyo alikuwa anahusishwa kujiunga na Yanga kabla ya kutambulishwa Simba hata hivyo utambulisho wa Heritier Makambo upande wa Timu ya Wananchi ulitoa ishara kuwa Simba ni Peter Banda.

Author: Asifiwe Mbembela