Simba yaipiga Yanga kijembe

Mgeni rasmi wa Mkutano Mkuu wa mashabiki wa klabu ya Simba Mussa Azan Zungu amewapiga na “Kitu kizito kichwani” kwa kauli ya lugha ya uswahilini baada ya kusema kuwa upande wa pili (Yanga) hawajui historia.

Zungu ambaye ni Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Bungeni amesema hayo wakati akitoa hotuba ya takribani dakika 15 mbele ya zaidi ya mashabiki 800 ambapo walijitokeza katika mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa JICC.

Zungu ambaye ni mgeni rasmi kwenye mkutano huo alitumia dakika 15 kuzungumza na moja ya vitu alivyozungumza ni kwamba baadhi ya watu wanaamini timu yao ndiyo ilishiriki kwenye uhuru wa Tanganyika.

“Hao hawajui historia ya nchi yetu, eti klabu yao imeshiriki kwenye uhuru,” alitania Zungu huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachama wa klabu hiyo.

Amesema viongozi waandaamizi wa Serikali akiwamo, aliyekuwa waziri mkuu, Rashid Mfaume Kawawa walikuwa ni wanachama wa klabu hiyo walioshirikiana ipasavyo na Mwalimu Nyerere.

“Wacha wajisifu tu, lakini Taifa letu ni moja na mwenyezi Mungu ni mmoja, lakini hawafahamu historia,” amesema Zungu.

“Maneno yalikuwa mengi ulipoteuliwa kuwa CEO, lakini umeonyesha unaweza na sasa wewe ni CEO uliyekubuhu, usiogope vijembe na maneno hayo yapo tu,”

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends