Simba yaitungua AS Vita Club 4-1 na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Klabu ya Simba imeibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya AS Vita Club katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi na kujikatia tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo mikubwa ngazi ya klabu.

Katika mchezo huo uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Leo Jumamosi Machi 3, Simba walikuwa wanahitaji alama moja tu kujihakikishia nafasi hiyo ambapo pointi tatu sasa zinawapa udhibiti wa msimamo.

Magoli ya Simba yametiwa kimiani na Luis Miquissone akimalizia pasi ya Clatous Chota Chama, kabla ya kusawazishwa bao hilo na Zemanga dakika chache baada ya lile la Simba.

Wekundu wa Msimbazi waliamuaka na kupata goli kupitia kwa kiungo mshambuliaji raia wa Zambia Clatous Chama aliyefunga goli mbili kabla ya Larry Bwalya kupigilia msumali wa mwisho na kufanya 4-1.

Baada ya matokeo hayo Simba inafikisha alama 13 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote hata hivyo wawataungana na Al Ahly wenye alama 8 wakati AS Vita akiwa na 4 na Al-Merrikh 3. Mechi ya Al-Merrikh na Ahly imeisha kwa sare ya 2-2.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares