Simba yajitutumua kusaka mrithi wa Chama Jr

140

Kikosi cha Simba Leo Agosti 14 Jumamosi kimemtambulisha Pape Ousmane Sakho raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 24 kuwa ingizo jipya la nne ndani ya Simba baada ya Jana Agosti 13 kumtambulisha Duncan Nyoni aliyeungana na Peter Banda pamoja na mchezaji mzawa Yusuph Mhilu

Nyota huyo anatajwa kuwa na uwezo mkubwa ndani ya uwanja pale anapopata nafasi akiwa ni kiungo mshambuliaji kinda aliyefanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Senegal.

Rekodi zinaonyesha kwamba alitupia mabao 8 na pasi 10 alitoa, pia ndiye mchezaji aliyeng’ara wakati timu ya Teungueth ikiitoa timu ya Raja Casablanca ya Morocco msimu ulioisha na kufuzu hatua ya makundi ya Caf Champions League.

Kwenye kambi nchini Morocco ambapo Simba wapo kwa sasa atajumuishwa na wengine ili kuendelea na maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.

Ujio wa mchezaji huyo ni baada ya kuondoka kwa Clatous Chota Chama pamoja na Luis Jose Miquissone ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Al Ahly ya Misri.

Author: Asifiwe Mbembela