Simba yampata mrithi wa Hans Poppe

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again amemtangaza Kassim Dewji kuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo.

Try Again ameweka wazi hilo wakati wa Mkutano Mkuu wa mashabiki wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Convertional Center JICC Jumapili Novemba 21.

Dewji anachukua nafasi ya Zacharia Hans Poppe aliyefariki dunia mwezi Septemba na kuzikwa kwao mkoani Iringa.

Katika mkutano mkuu wa klabu hiyo leo Jumapili, Try Again amesema bodi imempendekeza Dewji kuchukua nafasi ya Poppe.

“Tunafahamu uwezo Dewji, hivyo bodi imemkabidhi jukumu la kuongoza kamati ya usajili ambayo ilikuwa ikiongozwa na Poppe enzi za uhai wake,” amesema Try Again.

“Ni mwanasimba mwezetu, ameifanyia mengi klabu yetu, tunaamini ataendelea mazuri hayo”.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends