Simba yanyamazishwa na Mwadui

218

Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara imeendelea tena leo Jumatano kwa michezo sita katika viwanja mbalimbali nchini huku kikosi cha Simba kikiwa kimeshindwa kufurukuta dhidi ya Mwadui.

Simba ambayo ndiyo vinara wa TPL wameangukia pua kwa kupoteza mchezo dhidi ya Mwadui Fc kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa Shinyanga.

Goli pekee la Mwadui limewekwa kimiani na Gerald Mathias mnamo dakika ya 32 kipindi cha pili kwa njia ya kichwa akimalizia krosi iliyopigwa kutoka upande wa kushoto na kulia mwa Simba.

Matokeo haya yanaifanya Simba ipoteze kwa mara ya kwanza msimu huu lakini ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi na alama zake 18.

Matokeo kwa ujumla:-

Mwadui FC 1-0 Simba SC (Gerald Mathias 32′)

Ruvu Shooting 1-0 KMC (Santos Mazengo 17’)

Kagera Sugar 2-0 Namungo FC (Frank Ikobela 12’, Yusuphu Mhilu 69’)

Mtibwa Sugar 2-1 Coastal Union (Dickson Mbekya 20’, Jaffary Kibaya 56’ : Dickson Daud OG)

Lipuli FC 2-1 Polisi Tanzania (Kenneth Masumbuko 34’, Paul Nonga 74’  : Mohamed Mkopi 73’)

Singida United 1-2 JKT Tanzania (Ramadhan Hashim 55’ : Danny Lyanga 36’, Adam Adam 41’). Singida United wanaendelea kupambana nafasi ya mwisho wakiwa wamecheza mechi tisa alama tatu tu

Author: Bruce Amani