Simba yasahau kipigo cha Yanga, yaibamiza Singida United 8 – 0

Baada ya kuchapwa goli 1-0 na Yanga, Klabu ya Simba leo ni kama imeamua kulipiza kipigo hicho kwa kibonde Singida United ambapo wameichapa goli 8-0 kwenye mchezo wa VPL uliopigwa dimba la Uhuru leo Jumatano.Simba iliingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0 na Yanga huku Sinigida United ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 2-1 na Tanzania Prisons jambo lililofanya timu zote zicheze kwa kukamiana.

Mshambuliaji wa raia wa Rwanda Meddie Kagere alianza kuifungia goli la kwanza timu yake dakika ya kwanza tu akimalizia pasi ya Mohammed Hussein na baada ya hapo mvua ya magoli ikashuka dhidi ya Singida United ambayo inakamata nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa VPL ikiwa na alama 12.

Strika huyo alifunga tena kwenye dakika ya 25, 41 na 71 pasi mbili za magoli akipokea kutoka kwa Hassan Dilunga.

Magoli mengine yakitiwa kimiani na Deo Kanda dk 12 kwa pasi ya Kapombe,na dk ya 18 pasi Bocco, John Bocco alifunga bao moja dk ya 19 na Sharaf Shiboub alifunga bao moja dk 59 kwa pasi ya Deo Kanda.Singida United ilimaliza ikiwa pungufu baada ya mchezaji wao Haruna Moshi ‘Boban’ kuonyeshwa kadi nyekundu dk 52 kwa kumpiga kiwiko Manula.

Ushindi huo unaifanya Simba kuwa nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28 huku Singida United ikiwa nafasi ya 20 baada ya kucheza mechi 28 na ina pointi 12.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends