Simba yashinda mechi ya kwanza Afrika Kusini

113

Mabingwa wa TPL Simba SC wameushinda mchezo wao wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Orbet Tvet wa Afrika Kusini kwa goli 4-0 katika mchezo uliofanyika leo Julai 23. Simba ikiwa bondeni Afrika Kusini kwa wiki moja sasa, imecheza mchezo wa kirafiki katika kujaribu mbinu za kocha wao Patrick Aussems zinafanya kazi kiasi gani hasa katika kutengeneza muunganiko mpya na wachezaji wengine wapya waliosajiliwa msimu huu 2019/20 kutoka maeneo mbalimbali dunia.

Goli za Simba zimefungwa na Nahodha wa kikosi hicho John Raphael Bocco “Adebayo” ambaye amefunga goli 2 katika ushindi wa goli nne. Wakati Bocco akifunga goli mbili, Mbrazil  Da Silva aliyejiunga na timu hiyo msimu huu amefunga goli 1 sambamba na kiungo mshambuliaji wa Kitanzania Hassan Dilunga amefunga goli 1. Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Wanarobo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu 2018/2019 nchini Afrika Kusini.

Author: Asifiwe Mbembela