Simba yatoa orodha yao ya mashindano ya CAF

Jopo la makocha wa klabu ya Simba SC limeyataja majina 25 yatakayounda kikosi cha timu hiyo katika mashindano ya klabu bingwa Afrika yanayotarajiwa kuanza mda mfupi baada ya ratiba ya michezo hiyo kutolewa na CAF.

Simba ambaye ni bingwa mtetezi wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 atashiriki kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika baada ya miaka minne kukosa kushiriki ikiwa inashindwa kuwa bingwa wa TPL.

Kikosi hicho kimeundwa na

Walinda mlango wawili: Aishi Manula, na Deogrutish Munishi ‘Dida’.

Mabeki: Shomary Kapombe, Mohammed  Hussein, Asante Kwasi, Nicolas Gjan, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Jurko Mushid, Yusuf Mlipili, Salim Mbonde.

Viungo: Jonas Mkude, Clatous Chama, Hassan Dilunga, Mo Ibrahim, Shiza Kichuya, Hamis said Ndemla, Mohammed Rashid, James Kotei, Hatuna Hakizimana Niyozima, Mzamiru Yasni na Paul Bukaba.

Na Washambuliaji Emmanuel Okwi, John Raphael Bocco, Meddie Kagere na Adam Salamba.

Katika kikosi hicho limekosekana jina la Marcel Kaheza ambaye Kocha Patrick Ausseums amethibitisha atamutoa kinda huyo kwa mkopo ili apate mda mwingi wa kucheza kutokana na kipaji alichonacho.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends