Simba yatoshana nguvu na Olympique Morocco

Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Tanzania Simba SC imeendelea na maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2021/22 kwa kucheza mechi ya pili ya kirafiki dhidi ya Olympique Club mtanange uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Huu unakuwa ni mchezo wa pili kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Didier Gomes Da Rosa ukiwa ni mwendelezo kabambe kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa na TPL.

Ule wa kwanza walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 dhidi ya FAR Rabat ya Morocco.

Kikosi hicho kinatarajiwa kurejea mwishoni mwa juma hili ili kuendelea na maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares