Simba yatoshana nguvu na Township Rollers ya Botswana

Simba SC imetoshana nguvu na Township Rollers ya Botswana kwa kutoka sare ya goli 1-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Bondeni Afrika Kusini leo Jumamosi Julai 27 kujiandaa na msimu ujao wa kimashindano.
Goli la Simba limepatikana kupitia kwa Mnyarwanda Meddie Kagere kunako dakika ya 58 ya kipindi cha pili, goli lilodumu kwa muda wa dakika 11 pekee.
Township Rollers ambayo itacheza na Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika walisawazisha bao hilo dakika ya 70 kupitia kwa Serameng.
Huu unakuwa mchezo wa tatu kwa Simba kucheza nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujiaandaa na msimu ujao, ambapo ilianza na Orbet TVET ilishinda mabao 4-0 na ilishinda mbele ya Platinum Stars mabao 4-1 kabla ya leo kulazimisha sare ya bao 1-1.
Jumla ya goli 9 zimefungwa kwenye mechi 3 za kirafiki huku ikiruhusu goli moja, mchezo wa mwisho wa kirafiki nchini Afrika Kusini itacheza dhidi ya Orlando Pirates kabla ya kurejea Dar es Salaam kucheza mchezo wa Simba Day Agosti 6 mwaa huu dhidi ya Dynamo Power ya Zambia.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends