Simba yazindua jezi za kutumiwa katika michuano ya kimataifa

Klabu ya Simba imezindua rasmi jezi mpya ambazo zitakuwa zinatumika kwenye michuano ya kimataifa ambayo klabu hiyo itakuwa inashiriki kwa msimu wa 2020/21.

Simba SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Tanzania VPL wao ndiyo wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo wamepangiwa kucheza dhidi ya klabu kutokea Nigeria Plateau United.

Simba itaanza kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya makundi kwa kucheza na Klabu ya Plateau United ya Nigeria Uwanja wa New Jos kati ya tarehe 27-29 Novemba mwaka huu. Na mtanange wa mkondo wa pili unatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 4-6.

Author: Asifiwe Mbembela