Singida United yamsajili mshambuliaji Mghana

Wanafainali wa michuano ya Azam Federation Cup maarufu kama Azam FA mwaka 2017, Singida United wamekamilisha usajili wa wachezaji wawili na kuwatangaza siku ya leo Juni 30 kupitia kurasa rasmi za timu hiyo kwa ajili ya Ligi kuu Tanzania Bara.
Singida United kupitia kurasa hizo zimemsainisha mshambuliaji Herman R Frimpong, 22, kutoka nchini Ghana kwa kandarasi ya miaka mitatu(3) pamoja na mlinzi wa pembeni wa Malindi ya Zanzibar, Muharami Salum Marcello, 24,  mkataba wa miaka miwili.
Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga kabla ya usajili huo alisema timu hiyo imekamilisha mahitaji ya ripoti iliyoachwa na kocha Felix Minziro kuhusu wachezaji gani wasajiliwe kwa msimu mpya wa 2019/2020.
Singida haikuwa na msimu mzuri kwenye msimu uliopita ikiwa imenusulika kushuka daraja kutokana na changamoto za kifedha lakini msimu huu inaonekana kuimarika kwa namna ilivyofanya usajili.
Mbali na usajili huo, Singida United ilifanya mchakato wa kusaka vipaji vya wachezaji watakaotumika msimu ujao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends