Sofapaka yalenga dimba la Afrika

Klabu ya Sofapaka itacheza kwenye soka la Bara Afrika, hayo hi matamshi ya kocha ya timu hio John Baraza ambaye anasema fainali ya tarehe 20 kati yao na Kariobangi Sharks itakuwa ya muhimu kuliko mechi nyinginezo walizowahi kushiriki.

Sofapaka inalenga kurejea kwenye soka ya Afrika baada ya kushiriki mara ya kwanza mwaka 2009 walipolitwaa taji la ligi kuu nchini Kenya. Ikiwa watawashinda Sharks wataiwakilisha Kenya kwenye michuano ya mashirikisho barani mwaka ujao.

Kariobangi kwa upande wao kama watafuzu itakua ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hio. Bingwa mtetezi wa Kombe la Ngao AFC leopards walikwatuliwa nje na Sofapaka kwenye nusu fainali.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments