Sofapaka yamteuwa Medo kuwa kocha wake mpya

170

Sofapaka wamemteuwa Mmarekani Melis Medo kuwa kocha wake mpya. Medo alikuwa akiinoa Nakumatt FC ambayo sasa inafahamika kama Mount Kenya United na inaamika amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya “Batoto Ba Mungu”.

Medo aliisaidia Nakumatt kurudi katika ligi kuu ya kandanda Kenya licha ya kuwa kikosi chake kilikuwa na matatizo ya kifedha ambapo wachezaji walicheza kandanda kwa miezi kadhaa bila kulipwa mishahara.

Nakumatt waliwashinda Ushuru katika mechi ya mchujo ya mikondo miwili. Medo anachukua nafasi ya John Baraza ambaye alichukua mikoba ya uongozi wa timu huyo kufuatia kujiuzulu kwa Sam Ssimbwa mapema msimu uliopita.

Author: Bruce Amani