Solari apata kipigo cha kwanza kama kocha wa Real Madrid

123

Ushindi wa mfululizo wa Santiago Solari kama kocha wa Real Madrid umewekewa kikomo kwa kupewa kichapo cha 3-0 na Eibar. Ulikuwa ushindi wa kwanza wa Eibar katika La Liga dhidi ya Real.

Muargentina huyo alipewa mkataba wa kudumu baada ya kushinda mechi zote nne mfululizo tangu alipochukua mikoba ya Julen Lopetegui. Real ilijikuta nyuma kupitia bao la mapema la Gonzalo Escalante kwa upande wa wenyeji. Serge Enrich kisha aliongeza la pili muda mfupi baada ya kipindi cha pili na Kike akafunga kazi dakika tano baadaye na kuwaweka Eibar pointi mbili nyuma ya nambari sita Real Madrid.

Author: Bruce Amani