Solskjaer ajigamba kuifunga Villarreal na kutwaa ubingwa wa Europa

233

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kushinda taji la Ligi ya Europa mbele ya Villarreal itakuwa ni dalili njema kuelekea mafanikio makubwa ya United siku za mbeleni.
United watacheza dhidi ya Villarreal katika Mji wa Gdansk, Poland, Jumatano hii ya Mei 26 majira ya saa nne usiku Afrika Mashariki
Solskjaer ambaye ni mshindi wa Ligi ya Mabingwa kama mchezaji bado hajafanikiwa kubeba Kombe lolote klabuni hapo kama kocha tangia alipoichukua timu hiyo mwaka 2018/19.
Akizungumzia mchezo huo utakaopigwa keaho, Solskjaer amesema “hii ni timu ambayo tumekuwa tunaijenga kwa miaka michache iliyopita na tunaendelea kuijenga, nadhani hapa ni moja ya hatua nzuri”.
United haijashinda taji lolote kwa miaka minne iliyopita lakini kocha huyo anasema tofauti na vipindi vyote wakati huu anaona ni sahihi kufanya hilo kwa kuifunga Villarreal ambao wamemaliza nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga.

Author: Asifiwe Mbembela