Solskjaer asema anawaheshimu AS Roma wakati akijiandaa kuiongoza Man United Europa League

Bosi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema hajawadharau wapinzani wao AS Roma wakati wakijiandaa na hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Europa mtanange utakaopigwa dimba la Old Trafford Aprili 29.

Baada ya kushinda mechi dhidi ya Granada hatua ya nane bora, Solskjaer alisema haoni upinzani mkubwa kutoka kwa vilabu vya Italia.

Baadhi ya mashabiki wa Roma waliojitokeza kwenye uwanja wa mazoezi, walibeba mabango yenye picha ya kocha huyo zikitoa kijeli kama malipizo kwake.

“Michezo yote huwa migumu sana, nimekuwa nikiwafuatilia ni timu nzuri, ingawa bado sijawafanyia uchambuzi”. Alisema Ole Gunnar Solskjaer. “Ni timu yenye historia kubwa Italia na Ulaya kwa ujumla.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Anthony Martial na beki wa England Phil Jones watakosa mchezo huo ingawa beki Eric Bailly atarejea kikosini.

Amesema kama Manchester United itashinda taji hilo itakuwa sawa na kutimiza ndoto zao kufuatia msimu uliopita kuishia hatua ya nusu fainali mara nne.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares