Solskjaer asema mashabiki wa Man United wataona utofauti

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema mashabiki wa timu hiyo wataona mabadiliko kiuchezaji kwenye timu hiyo kuanzia kwenye mechi ya leo Jumamosi Novemba 20 dhidi ya Watford.

Ole Gunnar Solskjaer anasema hayo baada ya kikosi hicho kupitia wakati mgumu wa matokeo ikiwa inashika nafasi ya 6 kwenye msimamo katika mechi 12.

Baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa, kocha Ole, 48, anasema kila mmoja anaonekana mwenye ari kubwa kuhakikisha tunarudi kwenye njie yetu ya ushindi.

“Wachezaji, Viongozi, Mimi mwenyewe na klabu inafanya kazi kwa ushirikiano kuhakikisha tunarudi kwenye njia zetu za ushindi”, alisema Ole Gunnar Solskjaer ambaye amekuwa akihusishwa kung’olewa klabuni hapo.

United imeshinda mechi mbili katika nne kwenye mechi 12 za mashindano yote huku mlinda mlango David de Gea akiwa shujaa kwenye mechi mbalimbali.

Vipigo vya aibu pamoja na kuwa nje ya kiwango hasa kwenye mechi ya Liverpool ambapo walipigwa goli 5-0, kabla ya kuchezea kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa majirani zao Manchester City.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends