Solskjaer asema United kusajili wachezaji watatu

24

Kocha Mkuu wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema anahitaji kuongeza nyota wapya watatu ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao ili kukifanya kuwa na makali zaidi ya msimu huu.
Kocha huyo ambaye msimu huu alikuwa katika ubora wake hasa mechi za ugenini ambapo hawajafungwa mchezo wowote kati ya 19 anahitaji kuongeza nguvu zaidi ili aweze kushindana na mpinzani wake mkubwa Manchester City na Liverpool.
Katika Ligi Kuu England, United imekamilisha msimu kwa kujikusanyia jumla ya pointi 74 ikiwa ni namba mbili huku City ikiwa ni namba moja na pointi zao ni 86.
Mchezo wao wa mwisho kwa msimu United ilishinda jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Wolves.
Kocha huyo amesema: “Kwa sasa tunaangalia kwenye kikosi chetu wachezaji gani watasalia hapa na ambao wanatakiwa kuondoka na pia wale watakaotoka kwenda kupata uzoefu.
“Matumaini yangu kuboresha kikosi changu, wachezaji wawili ama watatu nahitaji ndani ya kikosi changu,”.
Chini ya Solskjaer, United imemaliza mara zote katika nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi nafasi ambayo inawapa uhakika wa kucheza michuano ya Ulaya.

Author: Asifiwe Mbembela