Solskjær atetea mbinu zake licha ya vipigo

97

Kocha Ole Gunnar Solskjaer wa Manchester United amesema hajaathirika na maoni ya baadhi ya wachambuzi ambao wanasema ili United ishinde mataji makubwa inahitajika kufanya mabadiliko ya kocha.

Solskjaer, 48, ameyasema hayo wakati akijibu hoja iliyotolewa na beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher aliyesema kuwa Manchester United wanahitaji meneja mpya ili kuwa washindani wa mataji.

“Sijaathirika hata kidogo, najiamini mwenyewe lakini pia klabu inaniamini. Ninauhakika kuwa maoni ya Jamie Carragher hayataenda kubadilisha chochote”, alisema kocha Solskjaer.

Solskjaer amekuwa kwenye presha kubwa hasa baada ya kupokea kipigo kizito cha goli 4-2 dhidi ya Leicester City mtanange wa Ligi Kuu England uliopigwa Jumamosi, kipigo ambacho sasa kinaifanya United kushinda mechi mbili, sare moja na kupoteza mechi nne katika mechi saba.

Manchester United wanarudi uwanjani Leo Jumatano kucheza dhidi ya Atalanta Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kumenyana na Liverpool wikiendi.

Author: Bruce Amani