Solskjaer atimuliwa Man United, kocha wa sita EPL kutimuliwa

Ni raundi 12 zimechezwe kwenye mbilinge mbilinge za Ligi Kuu England tangia kuanza kwa msimu 2021/22. Katika mechi hizo kumi na mbili tayari makocha sita wamefurushwa mizigo yao kutokana na matokeo hasi, wakati kipindi kama hicho msimu uliopita alikuwa ni kocha mmoja tu aliyefutwa kazi.

Kocha wa sita kufutwa kazi ni Ole Gunnar Solskjaer ambaye alikuwa anakinoa kikosi cha Mashetani Wekundu Manchester United kwa takribani miaka minne baada ya kupata kazi rasmi mwaka 2019, kabla ya hapo alikuwa anafanya kazi ya muda kuanzia 2018 baada ya kuichukua timu kutoka kwa Jose Mourinho.

Man United wametangaza leo Jumapili Novemba 21, 2021 kuwa hawataendelea na Solskjaer baada ya kuwa na wakati mgumu zaidi kwenye miezi miwili hii ambapo mbali na kupoteza mechi pia kiwango cha ubora wa uchezaji kilikuwa chini kabisa ,wakipoteza bao 4-1 kwa Watford.

Akipoteza kwa Manchester City 2-0, Liverpool 5-0, kutolewa na West Ham United Kombe la Ligi na kushinda mechi moja kati ya saba za ligi kuu ni moja ya mambo ambayo uongozi wa klabu hiyo umesema hauwezi kuendelea kumvumilia mtoto wa nyumbani, Ole.

Moja ya sababu ya kuwa na matokeo mabaya kwa United ambayo ilikuwa vizuri kipindi Ligi inarejea kutoka kwenye mapumziko ya Uviko-19 ni kurudi kwa mashabiki ambao wamekuwa wakiongeza hamasa kwa timu pinzani upande mmoja lakini upande mwingine mashabiki wamekuwa wakizomea timu ikifanya vibaya jambo ambalo viongozi hawapendi kulisikia.

Makocha wengine ambao wamefutwa kazi epl baada ya raundi 12 ni Xisco Munoz wa Watford, Steve Bruce wa Newcastle, Nuno Espirito Santo wabTottenham, Daniel Farke wa Norwich City, na Dean Smith wa Aston Villa.

Msimu uliopita ni makocha wanne tu waliofutwa kazi msimu mzima wakati kabla ya sikukuu za mwishoni mwa mwaka (christmas na mwaka mpya) ni kocha mmoja tu ndiye aliyefutwa kazi Slaven Bilic alikuwa West Brom.

Licha ya kiasi kikubwa cha fedha ambacho kimetumika katika madirisha ya usajili (pauni milioni 400) tangia United kuwa chini ya Ole Gunnar Solskjaer bado hayakuweza kusaidia timu hiyo kubeba hqta taji maoja ambapo mafanikio makubwa yalikuwa kushika nafasi ya pili kwenye Ligi msimu uliopita na kucheza fainali ya Europa ligi na kupoteza kwa Villarreal.

Katika kipindi hicho wachezaji kama Harry Maguire, Jadon Sancho, Raphael Varane, Aaron Wan-Bissakq, Bruno Fernandes, Cristiano Ronaldo, Edison Cavani, Donny van de Beek, Daniel James, Alex Telles, Facundo Pellistri na Diallo Amad.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends