Son ajifunga Tottenham Hotspur miaka minne

Winga wa Tottenham Hotspur Son Heung-min ameingia kandarasi mpya ya miaka minne kuendelea kukitumikia kikosi hicho mpaka mwaka 2025.

 

Son, 29, amefunga bao 107 katika mechi 280 tangia alipojiunga na timu hiyo kutokea Bayer Leverkusen mwaka 2015.

 

Ameitumikia timu ya taifa ya Korea Kusini mechi 93 na kufunga goli 27 katika mashindano mawili ya Kombe la Dunia.

 

“Sikuwa na maamuzi mengine tofauti ya haya, ilikuwa rahisi kwangu. Ninafuraha kuendelea kuwa hapa, nitakuwa mwenye furaha kuonana na mashabiki wetu tena” alisema Son.

 

Mkurugenzi wa Michezo Spurs Fabio Paratici ameongeza kuwa kila mmoja anajua thamani ya Son, akisema anamchango chanya kwenye matokeo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends