Sony Sugar yatimuliwa katika ligi ya Kenya

56

Sony Sugar wamefurushwa rasmi kutoka Ligi Kuu ya Kandanda Kenya – KPL, baada ya wao kushindwa kucheza mechi tatu za msimu huu wa ligi.

Kutokana na hilo, matokeo yao yote ya msimu huu yamefutwa na mechi zao za msimu kufutwa.

Siku ya Jumatano, Sony waliwapa Zoo Kericho pointi tatu za bure, baada ya kufanya hivyo pia kwa Tusker FC na AFC Leopards hapo awali.

Hatua hiyo inakuja licha ya juhudi ya klabu hiyo inayokabiliwa na matatizo ya kifedha kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Author: Bruce Amani